6 Juni 2025 - 21:33
Source: Parstoday
Baqaei: Kujaribu kuhalalisha jinai za kutisha za Israel ni janga kubwa zaidi duniani leo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Kujaribu kuhalalisha jinai za kutisha na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina, ni janga kubwa zaidi duniani leo, na kwamba waungaji mkono wa jinai hizo na wahalalishaji wa uhalifu wa kuchupa mipaka wa utawala wa Kizayuni ni washirika wa moja kwa moja wa jinai za Israel.

Shirika la Habari la Mehr limemnukuu Ismail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, akiandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: Ukweli wa mambo ni kuwa hata neno Palestina kwenye shati la mwakilishi wa Bunge la Ujerumani linaonekana kutovumilika na hiyo ni ishara tosha ya unafiki wa kimfumo wa wale wanaodai kuunga mkono juhudi za kuundwa nchi huru ya Palestina.

Amesema: Kuhalalisha mauaji ya kimbari ya Israel ni janga kubwa zaidi duniani hivi sasa, na waungaji mkono na wahalalishaji wa jinai za utawala huo ghasibu wa Kizayuni ni waitifaki na ni washirika wa jinai za Israel.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha